Mabeste na mkewe kwenye ‘Usiwe Bubu’

0
1064

MabesteNA SHARIFA MMASI

MSANII wa hip hop nchini, William Ngwi ‘Mabeste’, anatarajiwa kuachia wimbo mpya alioimba peke yake utakaotamba kwa jina la ‘Usiwe Bubu’.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mabeste alisema lengo la wimbo huo ni kuelimisha jamii kuwa na desturi ya kuweka mambo wazi ili kupata ufumbuzi utakaowatatulia matatizo.

“Niko njiani kuachia ngoma mpya itakayosikika masikioni mwa mashabiki kwa jina la ‘Usiwe Bubu’ ambayo nimeimba bila kumshirikisha mtu.

“Natoa wito kwa mashabiki wa kazi zangu, kukaa mkao wa kula kuupokea wimbo huu wenye mafunzo yatakayowasaidia kubadili maamuzi yao ya usiri na kuwa wawazi katika jamii,” alisema Mabeste

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here