30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Maajabu ya karoti katika kutibu magonjwa ya macho

Karoti

Na MWANDISHI WETU,

MATATIZO mengi yanayowapata watu leo hii kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na ulaji usiokuwa mzuri na kutozingatia kanuni bora za afya.

Watu wengi wamekuwa wakila kwa mazoea kwa maana ya milo mitatu kwa siku lakini linapokuja suala la mlo gani alioupata mtu husika ndio penye tatizo.

Mtu anaweza kumaliza siku nzima bila kugusa hata kipande cha tunda au kunywa juisi ya tunda husika.

Kulingana na wataalamu matunda yana virutubisho vingi mwilini na iwapo yatazingatiwa huwa ni kinga na tiba ya maradhi mbalimbali.

Karoti watu wengi wanaifahamu kama kiungo cha mboga lakini ni lazima tutambue kuwa karoti pia ni tunda.

Licha ya kuitumia kama kiungo katika chakula, pia unaweza kuitumia kama tunda kwa kuitafuna au kuisaga na kunywa juisi yake.

Karoti ina protini kidogo na haina mafuta kama yalivyo matunda mengine.

Pia ina asili ya wanga na ni chanzo kizuri cha vitamini B, C na E.

Aidha ina madini mengi ikiwemo madini ya chuma. Kuna kitu kinaitwa beta – rotene ambayo imo ndani ya karoti, hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamini A.

Vilevile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa kukinga kuta za utumbo.

Karoti inasaidia kukinga na kuponya magonjwa kama macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu, ngozi, kupunguza tindikali inayodhuru tumboni na kukinga magonjwa yenye asili ya kansa.

Karoti inaweza kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile, ikiwa mbichi kwa kutafuna, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga zingine.

Karoti pia inaweza kusagwa na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye saladi ya matunda  na mbogamboga.

Machicha ya karoti iliyosagwa yanaweza kutumika kama dawa kukinga ama kuponya maradhi ya nje ya mwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles