24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maafisa Biashara watakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) leo Mei 11, 2023 imeendelea kutoa mafunzo kwa siku ya pili kwa Maafisa Biashara kutoka katika Mikoa 10 ya Tanzania Bara.

Katika Mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Mtwara, Maafisa Biashara wamepitishwa katika vifungu 34 vya Sheria ya Leseni za Biashara (Sura 208) ili kuelewa tafsiri yake na namna ya kuvisimamia wakati wa utetekelezi wa majukumu katika maeneo yao ya kazi.

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Mkuu wa Sehemu ya Leseni za Biashara kutoka BRELA, Bw. Tawi Kilumile ameeleza kuwa Sheria hiyo ndio mwongozo mkuu wa utekelezaji wa majukumu yao kwakuwa umetoa uelekeo kuhusu nini cha kufanyika katika kila hatua.

“Sheria hii inatafsiri yake, kuanzia kifungu cha kwanza (1) hadi cha 34. Pia imeonyesha majukumu ya kila anayehusika katika kutekeleza Sheria hii, hivyo ni vyema tukaielewa vizuri na endapo kuna eneo lenye changamoto ni vyema kuuliza ili kupata uelewa wa pamoja,” ameeleza Kilumile.

Ameeleza kuwa tangu kupitishwa kwa Sheria hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 1972, imefanyiwa mabadiliko mara kadhaa, ili kuendana hali iliyopo hivi sasa, hivyo ni muhimu kuipitia mara kwa mara na kuielewa vizuri.

Kwa upande wake Afisa Leseni kutoka BRELA, Peter Riwa, amewataka Maafisa Biashara kutumia mbinu mbadala za kuwahamasisha wafanyabiashara kutii sheria na kuwa na Leseni badala ya kufungia biashara zao.

Ameeleza kuwa ni vyema wafanyabiashara wakaelimishwa kuhusu Sheria hii ili wafahamu kuwa kuna faini kwa mujibu wa sheria kwa kutokuwa na Leseni hivyo ni vyema kutii sheria ili kuepuka Usumbufu.

Akichangia mada katika mafunzo hayo, Afisa Leseni kutoka BRELA, Koyan Aboubakari, amewataka Maafisa Biashara kuwasaidia wafanyabiashara kufahamu jinsi ya kupata mahitaji muhimu kwa ajili ya kupata Leseni badala ya kukataa maombi yao.

Mahitaji hayo ni pamoja na namba ya Kitambulisho cha Taifa ya mwombaji wa leseni, namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), Uthibitisho wa sehemu ya kufanyia biashara kama mkataba wa pango, leseni ya makazi au hati.

Mahitaji mengine ni hati ya kuonyesha kutodaiwa kodi (Tax Clearance Certificate) Kibali kutoka mamlaka ya udhibiti (Kutegemea na aina ya biashara).

Kwa kufanya hivyo watakuwa wanafanikisha lengo kuu la serikali la kukuza biashara na kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles