Na Safina Sarwatt,Siha
Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Wazee na Watoto imejenga Maabara ya kisasa yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 11, itakayokuja na majibu ya changamoto ya maradhi yanayotokana vimelea mwenendo vya magonjwa yanayoambukizwa hapa nchini.
Mganga Mkuu wa Hospital ya taifa ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) Kibong’oto Dk. Riziri Kisonga aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akitoa taarifa ya ujenzi wa Maabara hiyo, kwa Kiongozi wa mbioy za Mwenge Maalum wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi.
Dk. amesema wa maabara hiyo itakapokamilika itatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa yanayoibuka na mapya ambayo ni hatarishi kwa usalama wa taifa na Kimataifa hasa tatizo kubwa sugu la vimelea kwa dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali.
“Nakupongeza sana Mkuu wa wilaya ya Siha Onesmo Buswelu pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Siha Ndahaki M’huli, kwa kazi za miradi yenu ambayo tumeitembelea, imeendana na thamani halisi ya fedha, zinzotolewa na serikali,” amesema.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu, alisema jumla ya miradi nane yenye thamani ya shilingi bilioni 21.7 ulitembelea na Mbio za mwengu, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya Msingi.
Mwenge maalumu wa Uhuru ulianza kukimbizwa mkoani Kilimanjaro Juni 5, mwaka huu, ambapo Juni 11 Mwenge huo utakabidhiwa mkoani Manyara.