22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kuchukua hatua kali Jumuiya zitakazokiuka sheria kujiendesha

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Serikali itazichukulia hatua kali Jumuiya zote zilizopo chini ya Wizara yake ambazo zitakiuka sheria na taratibu katika kujiendesha.

Akizungumza leo June 10, mwaka huu Jijini hapa na  Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO),Waziri Simbachawene amesema wale ambao wamekuwa na utaratibu wa kuleta vurugu na kuzivuruga Jumuiya,Wizara yake itachukua hatua kali ambapo amedai ikiwezekana hata pingu zitatumika.

“Ikipidi pingu itatembea haiwezekani mtu akawa anavunja sheria halafu anangaliwa tu na Mimi nitatuma Vyombo vya kufanya uchunguzi na tutachukua hatua kali kwa sababu wamekiuka Sheria za nchi.

“Songeni mbele atakaeleta shida mimi ndio nitakaeshughulika nae na salamu hizi ziwafikie jumuiya hizi zinaundwa kwa mujibu wa sheria za nchi haiwezekani watu wakawa wanafanya fanya masihara tutachukua hatua kali kwa wale ambao wanavuruga vuruga,” amesema Simbachawene.

Amesema Jumuiya hizo zilizoanzishwa na  zinazofanya mambo mazuri katika Nchi haiwezekani mtu mmoja akaleta  ugumu hivyo Wizara  itachukua hatua za kisheria na mwenye kuchukua hatua hizo ni yeye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Alfred Luvanda amesema wanamshukuru Waziri kwa kusimamia zoezi la  uchaguzi  wa kuwapata  viongozi wapya wa Shirikisho hilo  halali ambapo amedai sasa watakuwa na uhuru wa kufanya Mambo yao pamoja na kuzungumza na Serikali namna gani wanaenda katika ubia wa uendeshaji pamoja shule nchini.

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Youstor Mtungi amesema,wanakabiliwa na Changamoto ya baadhi ya wenye shule kuchukuliwa kama wafanyabiashara kwa kutozwa kodi nyingi wakati wao wapo kwenye lengo la kutoa huduma ya kumsaidia mtoto yoyote wa Mtanzania 

Amesema lengo lao ni kukaa na Serikali ili waone jinsi gani wanamsaidia mtoto wa Kitanzania ambapo amedai wanatambua lengo la kutoa elimu ni wajibu wa Serikali kwa kila mtoto wa Kitanzania lakini wao watasaidiana ili kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa na ubora.

Hata hivyo,aliwakaribisha wamili na shule binafsi kujiunga na Shirikisho hilo ili waweze kuzitatua Changamoto kwa pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles