24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Startimes na K4S waahidi kuboresha fursa kwa vijana

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Vijana wahimizwa kukimbilia milango ya fursa hasa katika Sekta ya michezo ili waweze kunufaika pamoja na kuinua michezo nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwa Televisheni mpya ya Tv3 itakayoonekana kupitia King’amuzi cha Startimes Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga mara baada ya kufunguliwa amesema kutokana na michezo kupewa nafasi kubwa kwenye jamii inaonyesha iko wazi kuwa kupitia sekta hiyo inaweza kufungua milango mingi ya ajira mbalimbali kwa vijana.

“Sehemu yoyote yenye michezo lazima kuwepo kwa fursa mbalimbali zenye kulenga kukwamua vijana kiuchumi, hivyo mimi kushirikiana na Startimes tumezindua rasmi Tv3 yenye maudhui ya michezo ili kujitangaza zaidi .”

Hata hivyo, Kusaga amesema ana lengo la dhati bado kuendelea kusaidia vijana katika soko la ajira katika tasnia ya habari na michezo kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Startimes, David Malisa ameeleza kwa jinsi gani Startimes wanavoendelea kuboresha huduma zao kwa kuwapatia wateja wao vitu vizuri na vyenye kukata kiu kuanzia michezo, filamu pamoja na tamthilia kwa lugha ya kiswahili.

“Tunaendelea kukuza na kuendeleza lugha yetu ya kiswahili hivyo utaona upo umuhimu wa kuwepo kampuni ya Startimes ili kupitia burudani kunaweza kuwepo na kuboresha lugha yetu yani kinyumbani zaidi,” amesema.

Malisa amesema Tv3 itapatikana kwenye lugha ya kiswahili ambapo maudhui yake ni ya kimichezo zaidi japo kutakuwepo na ‘Reality show’ pamoja na tamthilia.

“Tv3 kwa sasa itatoa nyanja ya kutangaza vitu vilivyopo nchini kwetu kimichezo na tamthilia hivyo itatupa fursa ya kutangaza utalii uliopo nchini kwetu hasa kukuza lugha yetu ya Kiswahili,” amesema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Ulinzi K4S Biko Scanda amehaidi kushirikiana na Kampuni ya Startimes kidhati ili kuhakikisha hali ya kiusalama zaidi katika Michezo.

“Kampuni yetu imekua miongoni mwa wadau wa michezo hasa mchezo wa ngumi na kuhakikisha ulinzi una imarika zaidi,”

Tunawapongeza Kampuni hiyo kwa kuendelea kutoa fursa za ajira mbalimbali kwa vijana kwani kuna baadhi ya vijana wengi wanajiingiza kwenye vitu vinavyohatarisha maisha yao na kupelekea kuwa vibaka.

“Kwa hiyo kupitia K4S pamoja na Startimes tunazingatia kuendelea kutoa fursa za ajira zaidi na tunategemea mechi ya ufunguzi wa Euro 2020 kesho katika uwanja wa Zakhiem tutaimarisha ulinzi wa kutosha,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles