32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watalii hifadhi ya Saanane waongezeka kwa asilimia 30

Na Sheila Katikula, Mwanza IDADI ya Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kilichopo ndani ya ziwa Victoria mkoani Mwanza imeelezwa kuongezeka kwa asilimia 30 na kufikia watalii 19,132 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa fedha 2020/2021  ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2019/20 ambapo takribani watalii elfu kumi pekee walitembelea  hifadhi hiyo.
Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane, Eva Mallya (katikati) akizungumuzia jambo na Maafisa wa Uhifadhi katika kisiwa hicho. PICHA Na Sheila Katikula, Mwanza.
Hayo yameelezwa na Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane, Eva Mallya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza hayo ni matokeo ya jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani na watu kutambua umuhimu wa  kufanya mazoezi, sanjari na kuunga mkono jitihada za serikali. Mallya amesema mbali na mafanikio yaliyofikiwa kwa mwaka wa fedha uliopita pia kwa kipindi hiki cha janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) uongozi wa hifadhi hiyo unatoa fursa ya watu kutembelea kwenye kisiwa hicho ili waweze kufanya  mazoezi  na kupumunzika sehemu yenye utulivu isiyo na mosongamano na kujiepusha na maambukizi ya UVIKO-19. Ameongeza ni vema wananchi kutumia fursa ya uwepo wa vivutio na mandhari mujaarabu yaliyopo kwenye kisiwa hicho kutembelea na watoto wao ili kuweza kukuza utalii wa ndani na kujifunza mambo mbalimbali na kuenenda na kauli mbiu ya Wizara ya Utalii kwa sasa isemayo ‘Tumerithishwa, Tuwarithishe’. Afisa Uhifadhi Wanyamapori na Mkuu wa kitengo cha Utalii wa Hifadhi ya Kisiwa Cha Saanane, Hilda Mikongoti  amesema hifadhi hiyo mbali na kuwa  wanyama mbalimbali ikiwemo simba,Swala, pimbi,Tumbili,Digidigi,Fisi Maji,Nyumbu,Pundamilia, Mamba Ndege pia kuna michezo ya watoto. Ameeleza, hifadhi hiyo ambayo ipo ndani ya ziwa victoria inatoa fursa ya watu kuweza kutalii kwenye ziwa kwa kutumia boti na kuangalia mandhari mazuri yanayozunguka kisiwa hicho.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles