28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Lwanga atamba kuendelea kutupia Simba

Na Mwandishi Wetu

KIUNGO wa Simba raia wa Uganda, Taddeo Lwanga,  amesema  anaamini ataendelea kuifungia timu yake   akipata nafasi ili kuisaidia kupata matokeo mazuri katika  mechi zake.

Lwanga ametoa kauli hiyo baada ya kufunga bao muhimu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini jana dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Lwanga alifunga bao hilo dakika ya pili baada ya kutokana na mpira wa kona uliopigwa na Rally Bwalya.

“Kama mchezaji najisikia furaha kufunga kwenye michuano mikubwa kama hii na kuisaidia timu kupata ushindi ugenini, binafsi naamini nitaendelea kufunga endapo nikipata nafasi,” amesema.

Hata hivyo amesema  bado hawatakiwi kubweteka kwa ushindi huo na kuwachukulia poa Galaxy katika mchezo wa marudiano kwani wana timu nzuri na katika  soka lolote linawezekana.

“Galaxy siyo timu mbaya, wako vizuri bado tunapaswa kuhakikisha tunachukua tahadhari ili kupata ushindi na kufuzu hatua ya makundi na hilo ndilo lengo letu,” amesema Lwanga.

Wekundu wa Msimbazi hao watashuka tena dimbani Jumapili hii katika mchezo wa marudiano dhidi ya Galaxy utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles