27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Lwandamina airejesha Yanga mchezoni

George Lwandamina
George Lwandamina

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

KOCHA mpya wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, George Lwandamina, jana aliwarejesha wachezaji wa timu hiyo mchezoni kwa kuanza mazoezi ya viungo yaliyodumu ndani ya saa 2:4, baada ya kuwa katika mapumziko ya wiki mbili tangu Novemba 11, mwaka huu.

Lwandamina alianza kazi rasmi saa mbili asubuhi jana, baada ya kuwasili Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es Salaam, akiwa sambamba na kikosi cha timu hiyo kilichokuwa na zaidi ya wachezaji 18.

Mara baada ya kufika uwanjani hapo akiwa na kocha msaidizi Juma Mwambusi, walionekana wakijadiliana kwa utulivu namna ya kuanza ratiba hiyo ya mazoezi.

Lwandamina alianza kwa kuwapa mazoezi mepesi ya viungo na kasi wachezaji hao, ambao walionekana kusikiliza kwa makini maelekezo ya kocha huyo wa zamani wa timu ya Zesco ya Zambia.

Wachezaji hao walianza mazoezi ya kukimbia kwa lengo la kupasha misuli na kuvifanya viungo viwe tayari kwa mazoezi na baadaye kupigiana pasi fupifupi 10 kwa kila mchezaji.

Ingawa mazoezi hayo yalionekana kuwa ya kawaida, yalichukua dakika 45 kwa kila hatua, kabla ya saa 3:45 asubuhi ratiba ya mazoezi hayo ilipomalizika.

Hata hivyo, miongoni mwa waliokuwapo katika mazoezi hayo ni sura mpya ya mchezaji kinda kutoka kituo cha wachezaji vijana cha Mbeya City, Goodlove Kwama.

Nyota huyo aliyekuwa majaribio ya wiki mbili akicheza nafasi ya winga wa kushoto, alionekana kujituma ili kumshawishi kocha huyo, ambaye muda wote alionekana akiteta jambo na Mwambusi.

Wakati huo huo, mshambuliaji mahiri wa timu hiyo, Mzimbabwe Donald Ngoma, anatarajia kuungana na wachezaji wenzake leo.

Ngoma, aliyekuwa mapumzikoni Zimbabwe, ataungana na wachezaji wenzake.

Mchezaji mwingine anayetarajia kuungana na kikosi hicho leo ni Malimi Busungu, ambaye saini yake inawindwa  na klabu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwamo Stand United na Tanzania Prisons.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles