25.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

LUPITA NYONG’O AIBUKA NA JAY-Z

LOS ANGELES, Marekani

STAA wa hip hop, Jay Z, ameachia video ya wimbo wake mpya, ‘MaNyfaCedGod’ aliomshirikisha James Blake.

Katika video hiyo ya wimbo unaopatikana katika albamu aliyoiachia hivi karibuni ya 4:44, Jay Z amemtumia mwigizaji mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong’o.

Jay Z amekuwa akiachia video kila wiki tangu alipoitambulisha 4:4:4 miezi miwili iliyopita.

Baadhi ya ngoma ambazo ameachia video zake ni pamoja na ‘4:44’, ‘Bam’ aliomshirikisha Damian Marley na ‘Kill Jay Z’.

Mpaka sasa ni nyimbo sita pekee ambazo msanii huyo hajazitolea video zikiwamo ‘Marcy Me’, ‘Family Feud’ na ‘Legacy’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,718FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles