29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Lukuvi kutekeleza agizo la JPM

Mwandishi Wetu – Dodoma

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Jumatatu atakwenda Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kurudisha umiliki wa ekari 750 kwa manispaa hiyo kama ilivyoelekezwa na Rais Dk. John Magufuli.

Rais Magufuli alitoa siku saba kuanzia Jumanne iliyopita kwa wizara hiyo kurejesha umiliki wa eneo hilo kwa Halmashauri ya Kigamboni baada ya kuufuta.

Alitoa agizo hilo baada ya kuzindua jengo la Manispaa ya Kigamboni na lile la mkuu wa wilaya eneo la Gezaulole, Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya mtandao jana akiwa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu anakohudhuria kikao cha mawaziri wa Afrika kuhusu masuala ya nyumba na maendeleo ya miji, Lukuvi alisema Jumatatu atakuwa ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kutekeleza agizo la rais kuhusu urejeshaji miliki ya ardhi kwa halmashauri hiyo.

“Jumatatu saa 5 asubuhi nitakuwa ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kutekeleza agizo la rais la kukabidhi ardhi ambayo iko katika eneo la Kigamboni,” alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli baada ya kufuta umiliki wa eneo hilo na kuwa chini ya Serikali, umiliki wake haujarejeshwa Manispaa ya Kigamboni na kutaka kurejeshwa ndani ya wiki moja ili wananchi wapange wanavyotaka.

Rais Magufuli alitahadharisha ardhi hiyo isije ikatumika vibaya kwani si ya viongozi, bali ni kwa maendeleo ya wananchi wa Kigamboni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles