24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Lukuvi ashusha kodi ya ardhi

LukuviNA MWANDISHI WETU, DODOMA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema wizara yake imehuisha viwango vya kodi, ada na tozo mbalimbali za ardhi kwa lengo la kupata viwango vinavyopangika.
Lukuvi alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana, wakati akiwasilisha makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2015/16.
Alisema kodi ya pango la ardhi imepungua kwa wastani wa asilimia 30 na viwango vingine vinavyomgusa mwananchi wa kawaida vimepungua kwa asilimia 50 au zaidi.
“Kwa mfano kodi ya kupima mashamba imepungua kwa asilimia 60, kutoka Sh 1,000 hadi Sh 400, na mashamba ya biashara imepungua kwa asilimia 50 kutoka Sh 10,000 hadi Sh 5,000 kwa ekari.
“Ada ya upimaji ardhi imepunguzwa kwa asilimia 62.5 kutoka Sh 800,000 hadi Sh 300,000 kwa hekta, nyaraka za tahadhari na vizuizi vimepunguzwa kwa asilimia 66.7 kutoka Sh 120,000 hadi Sh 40,000, nyaraka za ubadilishaji wa majina zimepunguzwa kwa asilimia 62.5 kutoka Sh 80,000 hadi Sh 30,000.
“Vilevile gharama za kupata nakala ya hukumu kwenye mabaraza ya ardhi zimepungua kwa asilimia 62.5 kutoka Sh 16,000 hadi Sh 6,000, ada ya kuomba umiliki wa ardhi imepungua kwa asilimia 75 kutoka Sh 80,000 hadi Sh 20,000,” alisema.
Aidha Lukuvi alisema pia ada za maandalizi ya hati imepunguzwa kwa asilimia 68.8 kutoka Sh 160,000 hadi Sh 50,000 ambapo viwango vyote hivyo vitaanza kutumika Julai Mosi mwaka huu.
Kwa upande wa tozo la mbele, kwa mwaka wa fedha 2015/16 itapungua kwa asilimia 50 kutoka asilimia 15 ya kiwango cha sasa hadi asilimia 7.5 ya thamani ya ardhi na kiwango hicho ndicho kitakacholipwa kwa mashamba na viwanja wakati wa kumilikishwa.
Kuhusu uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, alisema Serikali imefanya mapitio na kurekebisha matangazo yake ambapo eneo la mpango limepunguzwa kwa kuondoa kata tatu za Pembamnazi, Kisarawe II na Kimbiji zenye ukubwa wa hekta 44,440 ambazo hazitakuwapo kwenye mpango, hivyo kubakia na kata sita zenye ukubwa wa hekta 6,494.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles