Lukuvi apata mpinzani jimboni

0
2243

William LukuviNA RAYMOND MINJA, IRINGA
JOTO la uchaguzi limeendelea kupanda baada ya mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Mhandisi Sebastiani Kayoyo (39) kutangaza nia ya kuwani ubunge katika
Jimbo la Isimani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Jimbo la Isimani linaongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza nia yake juzi, Mhandisi Kayoyo alisema amepania kuhakikisha anaongeza kasi ya maendeleo na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wake.
Alisema si kwamba Waziri Lukuvi hajafanya mambo ya msingi, bali ameongoza jimbo hilo kwa muda mrefu, hivyo vijana walioko ndani ya CCM wanaweza kushika hatamu ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here