29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

‘LOWASSA YUPO KWENYE KIFUNGO CHA SIASA’

8qspaak9
Edward Lowassa

 

Na Mwandishi Wetu-Tabora

KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Khamis Mgeja, amewaomba Watanzania kumsamehe bure Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho,  Edward Lowassa kwa kushindwa kuwafikia kupitia mikutano ya kisiasa kwani yupo kwenye kifungo cha kisiasa.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Tabora, alipokuwa akizungumza na wanachama na viomgozi wa chama hicho katika kikao.

Alisema anasikitishwa kwa Lowassa kuzuiwa kuwashukuru waliompigia kura kupitia mikutano ya hadhara.

“Lowassa anapenda sana kuwafikia wananchi kwa kupitia mikutano ya hadhara, lengo lake lilikuwa ni kushukuru wananchi ambao walimpa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita na hiyo ilikuwa heshima kubwa waliyompa wananchi kwa yeye binafsi na Ukawa,” alisema Mgeja.

Alisema kwa Lowassa kamwe hatachoka kuwasemea wananchi kuhusu kero zao na ana imani kero hizo anazozisemea Rais Dk. John Mgufuli na viongozi wa CCM wanazisikia.

Kada huyo wa Chadema aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, alisema wananchi wanapaswa kumwelewa Lowassa na Ukawa kwa ujumla kuwa wanapenda kufanya mikutano ya hadhara.

“Sisi wachambuzi wa kisiasa tunaona dhahiri kabisa ishara ya kifungo cha kisiasa kwa Lowassa na viongozi wa vyama vya upinzani nchini kinachofanywa na watawala kwa kuminya demokrasia nchini,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles