23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Lowassa: Safari ya matumaini bado inaendelea Monduli

Pg 1 coolNA FREDY AZZAH, MONDULI

MGOMBEA Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema safari ya matumaini ilianzia Monduli Mkoa wa Arusha na itaishia Monduli.

Kutokana na hali hiyo  amewataka wananchi wapendane kwa sababu kuna maisha baada ya uchaguzi.

Lowassa aliyasema hayo jana kwa nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya kampeni   katika Jimbo la Monduli.

Akiwa Monduli mjini kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa polisi ambako ndiko nyumbani kwake, Lowassa alisema huku akishangiliwa:

“Safari ya matumaini ilianzia Monduli na itamalizikia Monduli”.

Akizungumzia suala la mtu atakayerithi kiti cha ubunge wa jimbo hilo aliloliongoza kwa miaka 20, Lowassa alisema kuna maneno mengi yanasemwa juu ya hilo lakini hawezi kuyasema sasa kwa kuwa atatafuta muda mzuri wa kuyasema.

“Kuna watu wanafikiri kwa kuwa nilikuwa CCM nitasaidia watu wa CCM, haiwezekani, nipo Chadema nitauza watu wa Chadema, NCCR, CUF na NLD na watu hao wasijaribu kutugawa.

“Kama nimekualika kwenye basi wewe ukachelewa hadi basi likaondoka, tusilaumiane. Najua watachukizwa na hatua hii na wana fedha nyingi, wakiwaletea fedha  kuleni lakini tusiwape kura hata moja, kuleni fedha zao.

“Wakiuliza jeuri tuliyonayo waambieni ni ya mshikamano na umoja, hata waje na fedha gani, Monduli iko imara naiacha imara,” alisema Lowassa.

Akiwa Loksale,  alisema ni kweli kuwa alipokuwa CCM alikubaliana na Mgombea ubunge wa   Monduli kupitia CCM, Namelok Sokoine, kuwa agombee kwenye jimbo hilo.

“Ni kweli tulikubaliana agombee, mabadiliko yalivyotokea, nikamwambia atoke, kama CCM hainitaki kwa nini abaki, mimi niko kwenye basi la Chadema siwezi kumbeba mtu wa CCM,” alisema.

Alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa Chadema kwenye mkutano wa Monduli mjini, Lowassa alitumia kifungu cha Biblia kumnadi mgombea huyo.

“Wale wanaosoma Biblia  kuna msitari unasema huyu ndiye mwanangu mpendwa niliyependezwa naye. Huyu ni mtu makini, amesoma, hatahongeka, ukirudi nyumbani waambie wenzako, mbunge ni Kalanga, tuwaambie maadui zetu wasome namba,” alisema.

Kuna maisha baada ya uchaguzi

Akiwa Engaruka Chini, alisema kwa muda aliokuwa kiongozi ikiwamo jimboni Monduli, alijenga umoja na mshikamano  hivyo hataki mtu wa kuuvuruga kwa kuwa anaamini kuna maisha baada ya uchaguzi.

“Sitaki mtu avuruge umoja wetu, tumefanya mambo yetu mengi kuna maisha baada ya uchaguzi  tuishi kwa amani na usalama, umoja na mshikamano ni muhimu,”alisema.

Aliwataka   wazee wa mila wa kabila la kimasai waitwao malaigwanani, waendelee na kazi yao ya kuongoza wenzao kwa haki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles