24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA AMLILIA CASTRO

Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Balozi wa Cuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo, Dar es Salaam jana wakati alipokwenda kumpa pole kutokana na kifo cha Rais mstaafu wa nchi hiyo, Fidel Castro.
Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Balozi wa Cuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez
Tormo, Dar es Salaam jana wakati alipokwenda kumpa pole kutokana na kifo cha Rais mstaafu wa nchi hiyo, Fidel Castro.

Na JONAS MUSHI – DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu wa zamani Edward Lowassa, amesema Cuba ni taifa dogo lililoitikisa dunia kwa sababu ya uongozi imara wa aliyekuwa Rais na mwanamapinduzi wa nchi hiyo, Fidel Castro.

Lowassa ambaye pia ni na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliyasema hayo jana Dar es Salaam, nyumbani kwa Balozi wa Cuba nchini, Jorge Luis Lopez Tormo, alipofika kumpa pole na kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Castro kilichotokea Novemba 25, mwaka huu jijini Havana Cuba.

Alisema kiongozi huyo ni mwanamapinduzi aliyemhamasisha kwa namna alivyokuwa akifanya kazi ya kuwatetea wanyonge na masikini kote duniani.

“Castro alikuwa mtu mwenye maono na misimamo ya kile alichokiamini na kuifanya Cuba pamoja na udogo wake itikise dunia, ukienda kila mahali unamsikia Castro… ni mwanamapinduzi aliyefanya kazi ya kuwatetea wanyonge na masikini na dunia ilimfahamu hivyo. Alini-‘inspire’ (hamasisha) kwa sababu alikuwa ‘focused’ na mwenye kusimamia kile alichokiamini,” alisema Lowassa.

Castro alikuwa mwanamapinduzi wa miaka ya 1950 ambaye alimpindua aliyekuwa kibaraka wa Marekani, Rais Fulgencio Batista mwaka 1959, baada ya kuendesha vuguvugu la watu waliokuwa tayari kuipinga Serikali iliyokuwa imetawaliwa na rushwa na anasa zilizofanywa na wawekezaji kutoka Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles