24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

LOLIONDO WAFIKISHA KILIO KWA WAZIRI MKUU

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

WANANCHI wa Loliondo wamefikisha kilio chao kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu uchomaji wa makazi na uondoaji wa wananchi wakidai ni kinyume na haki za binadamu.

Nakala ya barua kwa Waziri Mkuu ambayo imebeba malalamiko juu ya tukio hilo ilisomwa mbele ya waandishi wa habari na mwakilishi wa wananchi hao, Kipilangati Kaura ambaye ni hsemu wanaotetea makazi yao.

Kaura na wenzake wamefika Dar es Salaam,  kwa ajili ya kufikisha malalamiko yao kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  huku wakiamini  watasikilizwa na kusaidiwa endapo kwa kuwa wanaendelea kupata mateso.

Alisema  wameamua kufanya hivyo huenda Waziri Mkuu hajui kile ambacho kinaendelea na kwa kumtumia Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na kudai kwamba kuna jambo la ukweli limepindishwa katika kuhamishwa kwao.

Katika nakala hiyo ya barua pia imemuelezea Waziri Mkuu kuhusu mgogoro huo kuwa ni wa zamani kwa takribani miaka 26 iliyopita na kwamba tayari jitihada mbalimbali za kuumaliza zimefanyika lakini  zimegonga mwamba kutokana na kutatuliwa kisiasa na kuangalia maslahi binafsi.

Alisema maboma mengi katika kata saba za tarafa ya Loliondo yamechomwa moto huku wananchi wa maeneo husika wakitakiwa kuondoka kwa nguvu kwa kile kinachodaiwa kupisha eneo la Hifadhi ya Serengeti.

Naye Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema Loliondo hali ni tete si tu kwa wananchi bali hata waandishi wa habari ambao wamekuwa wakifanya kazi zaokwa kuiba.

Alisema wananchi walioathiriwa wanatakiwa kuwa watulivu na kufanya suala hilo kwakufuata utaratibu wa kisheria ili haki ipatikane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles