27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Liverpool yatinga nusu fainali Capital one

5440e5ea639b3LIVEPOOL, ENGLAND

KIKOSI cha kocha Jurgen Klopp, Liverpool, imekuwa timu ya mwisho kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Capital One.

Klabu hiyo imeingia hatua hiyo baada ya kuichapa timu ya Southampton kichapo kitakatifu cha mabao 6-1.

Southampton walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema katika dakika ya kwanza ya mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake, Sadio Mane na kuanza kuwachanganya wapinzani wao, lakini mfumo wa Klopp uliweza kubadilisha matokeo.

Mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge, ambaye alikuwa benchi kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi, alifanikiwa kuisawazishia timu yake katika dakika ya 29, kabla ya mchezaji huyo kuongeza bao la pili.

Mshambuliaji Divock Origi akaongeza mabao matatu katika dakika ya 45, 68 na 86, huku Jordan Ibe naye akifunga bao moja na kukamilisha idadi ya mabao 6.

Michezo ya nusu fainali ya kwanza itafanyika Januari 5 na 6 na michezo ya marudio ikifanyika 25 na 26 ambapo Liverpool watachuana na Stoke City katika mchezo wa nusu fainali, huku Manchester City wao wakikabiliana na Everton.

Klopp amesema kikosi chake kina nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa michuano hiyo kutokana na dalili walizozionesha katika mchezo huo.

“Hatuna maajabu makubwa, lakini mifumo yetu itatufanya tufanikiwe kuchukua ubingwa wa Capital One, tunajituma sana na ndiyo maana tunaamini tunaweza kuchukua ubingwa msimu huu,” alisema Klopp.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles