29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

LISSU: UCHAGUZI WA KENYA DARASA

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu, amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Kenya unawafundisha Watanzania umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya.

Lissu alitoa kauli hiyo jana wakati akihojiwa na mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha televisheni hapa nchini.

Alisema kwamba uchaguzi huo unawafundisha Watanzania kuwa na Katiba ya kidemokrasia ambayo inaweka uhuru kwa washiriki wa uchaguzi, utaratibu wa kushiriki na kufahamu matokeo ya uchaguzi.

“Uchaguzi wa Kenya unatufundisha umuhimu wa kuwa na demokrasia, tumeona wafungwa wakipiga kura, tumeona waandishi wa habari wakiingia gerezani kueleza umma jinsi ambavyo zoezi la upigaji kura linavyoendelea, hata kwa wale ambao wamepata adhabu za kifungo cha sheria kwa mujibu wa sheria za Kenya, lakini kwetu sisi  hicho kitu hakipo kabisa.

“Tumeona raia wanaokaa nje ya Kenya wameshiriki uchaguzi, sisi hilo haliwezekani na yote nasema ni  funzo kubwa la kuwa na mfumo wa kidemokrasia,” alisema.

Alipoulizwa sababu za Chadema kuunga mkono muungano wa Jubilee wakati wa kampeni, Lissu alisema si kitu cha ajabu kwa chama chake kuwa na chama rafiki Kenya.

Alisema Chadema kina chama rafiki Ghana ambacho ndicho chama tawala. Pia kina vyama rafiki kila mahali.

“Wakati wa uchaguzi, marafiki wanaungana mkono, Frelimo wanaunga mkono CCM, ANC wanaunga mkono CCM na chama tawala cha Uganda kinaunga mkono CCM.

“Sisi tunaunga mkono muungano wa Jubilee kama ambavyo mwaka 2013 tuliunga mkono ODM ya Raila Odinga, lakini baada ya uchaguzi ule na uchaguzi wa kwetu wa mwaka 2015, Raila ambaye tulimuunga mkono sisi wakati ule akawa ndiyo chanda na pete na Rais Magufuli.

“Na kwenye uchaguzi wa Kenya juzi, Raila Odinga aliwaambia Wakenya kwamba wakimchagua ataendesha nchi ya Kenya kama Magufuli. Ilibidi tuwaambie Wakenya kwamba mtakoma,” alisema Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles