23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC, THRDC na Save The Childern waratibu uandishi wa ripoti ya haki za binadamu

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC) pamoja na Shirika la Save The Children kimeratibu uandishi wa pamoja wa ripoti ya wadau kuhusu tathimini ya hali za binadamu na kuitumia katika Baraza la Umoja wa Maataifa la Haki za Binadamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga(kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari, kushoto Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Wakili Onesmo Olengurumwa.

Akizungumza leo Dar es Salaam Alhamis Aprili mosi, 2021 Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga, amesema ripoti hiyo ni zao la ushirikiano wa asasi 228 zinazofanyakazi nchini.

“Ripoti hii imejumuisha masuala mbalimbali ya haki za binadamu kwa kuzingatia mapendekezo 133 yaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2016 na kukubaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuyafanyia kazi katika kipindi cha miaka minne (2016-2021).

“Kiufupi mchakato wa tathimini ya hali ya haki za binadamu (Universal Periodic Review) huwa unafanywa na Baraza la Umoja wa Mataifa  la Haki za Binadamu, ambapo hufanya mapitio ya taarifa mbalimbali kuhusu hall ya haki za binadamu kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha miaka mine.

“Baada ya kufanya tathmini hiyo, Baraza hutoa mapendekezo kwa nchi husika kuboresha hali ya ulinzi wa haki hinadamu ambapo Tanzania kwa mara ya kwanza ilifanyiwa tathimini mwaka 2011 na 2016, kwa kipindi hiki baraza linatarajia kufanya tathimini Novemba, mwaka huu. Hivyo asasi za kirai zimepewa nafasi ya majukumu ya kusaidia Baraza kupata taarufa kuhusu hali ya haki za binadamu kwa kuzingatia miongozo waliyoitoa,” amesema Wakili Henga.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema mchakato wa ufuatiliaji na baadaye uandikishaji wa ripoti hiyo ulianza tangu mwaka 2016 baada ya tathimini ya hali ya haki za binadamu iliyofanyika Geniva (Uswizi).

“Mwaka huohuo 2016 Asasi za Kiraia ziliandaa mpango kazi wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo yaliyokubaliwa na Serikali yetu.

“Mwaka 2019 wadau wa Asasi za Kiraia waliwasilisha ripoti nyingine ya ufiatiliaji katika kipindi cha miaka miwili (UPR Midrterm Report), Mikutano mingine ya ufuatliaji iliendelea kufanyika mara kadhaa ikihusisha pia wawakilishi wa serikali, huku hatua ya kuandaa mpango kazi wa AZAKI kuhusu ufuatiliaji utekelezajiwa mapendekezo hayo ukipongezwa na Wizara ya Katiba na Sheria,” amesema Olengurumwa na kuongeza kuwa;

“Mchakato huu wa tathiminiya haki za binadamu unahusisha utekelezaji wa mapendekezo 133 yaliyotolewa na Barza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamukwa Tanzania. Hivyo katika ripoti yetu, utekelezaji wa asilimia 89 ya mapendekezo yote yaliyotolewa haujakamilika kwa asilimia 100,” amesema Olengurumwa.

Ameongeza kuwa mapendekezo hayo ji yale yanayohusus haki za wananwake, watoto, haki za uchumi, haki za kijamii na watetezi wa haki za binadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles