CAF yaruhusu Mashabiki 10,000 kuzitazama Simba, Namungo

0
370

Dar es Salaam, Tanzania

Shirikisho la Soka Afrika(CAF), limeruhusu mashabiki 10, 000 katika mechi za Simba na Namungo, zitakazochezwa wikiendi hii, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Simba inatarajia kucheza na AS Vita ya DR Congo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Namungo itacheza na Nkana ya Zambia Jumapili mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.

CAF imeruhusu mashabiki hao kutokana na maombi ya Shirikisho la Soka Tanzania baada ya michezo iliyopita timu hizo kucheza bila mashabiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here