27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

LATRA Mwanza yaombwa kufuta nauli za zamani

KAMATI YA SIASA ILEJE YATOA 2,000,00 KWA FAMILIA ZILIZOPOTEZA WATU 5.
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ileje mkoani Songwe imefanikiwa kuzitembelea familia zilizopoteza ndugu watano wa familia mbili tofauti  aliwepo mama mjamzoto wa mimba ya miezi tisa katika kata ya Sange na Ngulugulu wilayani humo.
Akizungumza kwaniaba ya kamati ya siasa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani humo Hebroni Kibona amesema kama chama wamefika Kwa ndugu hao lengo likiwa ni kiwafariji na kuwapa mkono wa pole, baada ya kupoteza ndugu zao.
Kibona amesema kamati ya siasa imefanikiwa kuchangishana fedha na kukusanya 2,000,00 ambapo Kwa Kila familia wametoa shilingi laki moja(1,000,00).
“Kama chama bado kinaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu kwao Kwa kupoteza ndugu zao ambao walipoteza maisha baada ya nyumba zao kubomoka Kwa kuangukiwa na magema ya milima katika Kijiji Cha Sange kata ya Sange na kijiji Cha Kisyesye kata ya Ngulugulu”, amesema Kibona.
Kibona amesema waliofariki katika tukio katika Kijiji Cha Sange mke ma mme pamoja na mtoto(4) huku mwanamke huyo akiwa na mimba ya miezi 9, ambapo kwa kata ya Ngulugulu Kijiji Cha Kisyesye wanafamilia wawili walifariki Dunia.
Katibu wa hicho wilayani humo Hassan Lyamba amesema kamati ya siasa imeungana na famalia hizo katika kipindi hiki kigumu Cha kupotelewa na ndugu zao, katika tukio lililotokea April 28, 2022, ambapo chama na serikali wapo sambamba na familia zao.
Katika kipindi Cha msimu wa mvua, amewasihi wananchi kuchukukua tahadhari ya mapema hususani tarafa ya Bundali ambapo udongo ni tifutifu ma kupelekea magema kupolomoka ,na maisha ya wakazi wa maeneo hayo kuwa hatarishi.
Diwani wa Kata ya Ngulugulu Joshua Swila akizungumza baada ya kupokea salamu hizo kwaniamba ya familia hizo,ameipongeza kamati ya siasa Kwa kuamua kutembelea familia zilizopoteza ndugu zao, kutokana na vifusi kuangukia nyumba zao, ambapo mawasiliano ya barabara kukatika, mifugo kama ng’ombe kufa na kuipongeza serikali kuwa na jitihada za kufungua barabara.
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi wilaya ya Ileje imefikia hatua hiyo baada ya usiku was kuamkia April 28,2022 watu 5 walifariki dunia akiwepo mama mjamzito was mimba ya miezi 9  kutokana na mvua kubwa kunyesha iliyopekea magema ya kifusi kuangukia nyumba, kukatika Kwa barabara na baadhi ya madaraja iliyopelekea baadhi ya wanafunzi kukosa masomo.
PICHA YA KWANZA MWENYEKITI WA CHAMA AKIKABIDHI FEDHA KWA KATIBU WA CCM KATA YA NGULUGULU KWANIABA YA FAMILIA.
PICHA YA PILI WAJUMBE WA KAMATI YA SIASA WILAYA ILEJE WAKIWA PAMOJA KATIKA MOJA YA FAMILIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles