25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wauguzi Kagera watakiwa kuendelea kusimamia maadili

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Wauguzi mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kusimamia maadili na misingi ya taaluma yao ili kujiepusha na kufukuzwa kazi na kuharibu ndoto zao.

Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Dk. Mustafa Waziri wakati akizungumza nawaandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani Mei 12, 2022 ambayo katika Manispaa ya Bukoba imefanyika katika kituo cha Afya Zamzam.

Maadhimisho hayo ya wauguzi yamefanyika sambamba na kiapo ambacho hua ni utaratibu wa kawaida katika siku kama hiyo ya wauguzi duniani na kwamba kiapo hicho kinawakumbusha ni namna gani wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa umakini na weledi.

Dk. Waziri amesema kuwa Kituo cha Afya Zamzam kimekuwa kikitoa huduma kwa wananchi wengi wa maeneo tofauti tofauti ndani na nje ya Bukoba na kusifiwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa na kwamba tangu kituo hicho kimeanza kutoa huduma za upasuaji, tayari wamefanya upasuaji zaidi ya 366 ambayo imekuwa ikinusuru wananchi wengi zaidi.

“Nitumie nafasi hii wahiyo na mimi niwapongeze wauguzi wangu kwa kazi nzuri wanazofanya katika kuboresha huduma katika kituo cha Zamzam,” amesema Dk. Waziri.

Nae Muuguzi Mkuu Mkoa wa Kagera, Mercy Obadia Kagaruki ambaye pia ni Msimamizi wa shughuli za Huduma na Ukunga Kagera amesema kuwa katika Mkoa wa Kagera wamejipanga kuboresha huduma na kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya mama na mtoto na kuwataka wauguzi wenzake kutoa huduma bora wakiwa kazini na kuwajibika kwa wananchi na kuwaona ni wamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles