29.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Lambert ang’aka bungeni, mtambo wa Barakoa MSD ulivyo itia hasara Serikali

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mbunge wa Viti Maalumu Agnesta Lambert amesema mtambo wa kutengeneza barakoa ulionunuliwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD) kwa zaidi ya Sh million 600 umeonekana kuitia hasara Serikali kwakuwa imeshindwa kutimiza malengo.

Aidha, mbunge huyo amesema kuwa serikali ilinunua mtambo huo kwa lengo la kuzalisha barakoa millioni 4 kwa mwezi lakini cha kushangaza mtambo huo mpaka septemba mwaka Jana ulizalisha barakoa 320,000 badala ya malengo yao ya kuzalisha barakoa 504 kwa mwezi.

Lambert aliyasema hayo Mei 11, 2021 bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto iliyowasilishwa Jana.

“Naiomba Serikali ifanye Uchunguzi wa kina kuhusiana na ununuzi wa huo mtambo wa kutengeneza barakoa wa MSD, tumenunua kwa pesa nyingi lakini cha kushangaza mtambo huo umekuwa ukizalisha chini ya kiwango,” amesema Lambert.

Aidha, Lambert alisema yeye amejikita katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) iliyosema mtambo ulionunuliwa kwa pesa nyingi lakini umeshindwa kukidhi malengo kusudiwa.

“Kwa mujibu wa ripoti ya CAG baada ya MSD kuona mtambo huo unashindwa kuzalisha idadi ya barakoa tarajiwa waliamua kununua compressor nyingine ambayo hata hivyo haikuweza kuzalisha barakoa walizokusudia Jambo lililopelekea wananchi kukosa barakoa za kujikinga dhidi ya Corona,” alisema Lambert.

Lambert alisema kutokana na sintofahamu hiyo, ameitaka Serika kufanya Uchunguzi wa kina,kujua kama kweli mtambo huo ulinunuliwa kwa pesa hiyo.

Aidha Mbunge huyo ameitaka Serikali kulipa deni la Sh billioni 256 wanalodaiwa na MSD ili waweze kuagiza dawa.

“Serikali imekuwa na usugu wa kulipa madeni ya MSD, bajeti iliyoidhinishwa mwka 2019,2020 ilikuwa Sh bilioni 200 lakini Serikali haikupeleka hata shilingi moja, hali inayopelekea MSD kushindwa kununua dawa na Vifaa tiba jambo linalohatarisha maisha na afya za Watanzania alisema Mbunge huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles