23 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Lamadi Utalii Festival kukusanya watalii, wajasiriamali zaidi 300

Derick Milton, Busega

Mkuu wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera amesemakuwa wilaya hiyo imeandaa tamasha kubwa la kukuza na kuendeleza Utalii uliopo na Kanda ya Ziwa kwa ujumla litakalofanyika kwa siku nne kuanzia Desemba 29 hadi Januari Mosi mwaka huu.

Mwera amesema kuwa tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Itongo Lamadi, ambapo linatarajia kushirikisha zaidi ya watalii na wajasiriamali 300.

Amesema katika ufunguzi wa tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Utalii , Constantine Kanyasu, huku siku ya kilele mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo Dk. Raphael Chegeni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 37, Mkuu huyo wa Wilaya amesema lengo la tamasha hilo ni kutangaza Utalii wa Kanda ya Ziwa ikiwemo Mji wa Lamadi pamoja na utamaduni wa mkoa wa Simiyu na Mara.

“Wilaya ya Busega tumekuwa tukipakana na hifadhi bora nchini ya Serengeti, lakini bado hatujaweza kuitumia katika kutangaza Utamaduni wetu, wananchi wa mji wa Lamadi kuitumia kufanya biashara, tuliona tuanzishe tamasha hili kuweza kujitangaza lakini pia wananchi wa Lamadi waweze kufanya biashara kupitia ujasiriamali wao wa kisanaa,” amesema Mwera.

Aidha amesema kuwa watalii kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti watakuwepo kuweza kuangalia utamaduni wa wasukuma, wasanii wa Sanaa mbalimbali za ususi, uchoraji na kuchonga huku akitangaza uwepo wa Utalii wa baiskeli, kutembelea Serengeti na Utalii wa Boti ziwa Victoria.

Mkuu huyo wa Wilaya ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wote wa Wilaya hiyo na kanda ya ziwa wenye ubunifu mbalimbali kujitokeza na kutangaza bidhaa zao kwani hakutakuwa na kiingilio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles