LOS ANGELS, MAREKANI
MWANAMITINDO bilionea nchini Marekani, Kylie Jenner, juzi alimliza mama yake Kris Jenner, baada ya kumnunulia gari aina ya Ferrari 488 kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Kris anatarajia kutimiza miaka 63, Jumatatu wiki ijayo, hivyo Kylie aliamua kuonesha jeuri ya fedha huku akitumia kiasi cha dola 250,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 571 za Kitanzania kununua zawadi ya gari kwa mama yake.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo aliandika: “Ferrari 488 ni kwa ajili ya mama yangu mrembo, siku zote alikuwa na ndoto ya kumiliki aina hiyo ya gari, hivyo ninaamini sasa ndoto zake zimekamilika,” aliandika.