26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kuungua moto nyumba ya Mkurugenzi Meatu, uchunguzi bado

Na Derick Milton, Meatu.

Tukio la kuungua Moto nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashuari ya Wilaya ya Meatu, ambalo lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 14, 2020, limeendelea kuchunguzwa na kamati maalumu ambayo iliundwa na Mkuu wa Mkoa.

Akiongea leo Desemba 8, mbele ya kikao cha kwanza cha Madiwani ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kuwaapisha, Mkurugenzi wa Halmashuari hiyo, Fabian Manoza amesema kuwa uchunguzi bado unaendelea kamati hiyo.

Manoza ametoa maelezo hayo, baada ya Madiwani wa halmashuari hiyo, kutaka kupewa majibu ya nini chanzo cha tukio hilo pamoja na mali ambazo ziliaribika, ambapo majibu yote yatatolewa na tume hiyo mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Aidha Mkurungenzi huyo amesema baada ya tukio hilo kutokea, Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka, aliunda kamati ya uchunguzi ambayo inaundwa na vyombo vya ulinzi na usalama, wakiwemo wataalamu kutoka Tanesco.

“ Mpaka sasa tume hiyo ambayo iliundwa na Mkuu wa Mkoa, haijatuletea nini wamekibaini, uchunguzi bado unaendelea, wakimaliza watatwambia na sisi tutapata majibu ya maswali haya na tutaletwa kwenu na tutatoa taarifa kwa wananchi,” amesema Manoza.

Usiku wa kuamkia Novemba 14, 2020 saa tisa alfajiri, Nyumba hiyo ya Mkurugenzi iliungua yote ziwemo na mali zote zilizokuwemo ndani, na hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa.

Hata hivyo wakati nyumba hiyo ikiungua, Mkurugenzi huyo Manoza alikuwa Safari na Familia yake, huku mdogo wake wa kiume ambaye alikuwemo ndani ya nyumba hiyo siku ya tukio, akifanikiwa kukimbia kujiokoa baada ya tukio kutokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles