26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima: Nasubiri kutumwa kazi

Na Faraja Masinde

Waziri wa mteule wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ambaye ameteuliwa na Rais Dk. John Magufuli amesema yupo tayari kufanya kazi kwa ajili ya kuona Tanzania inapiga hatua kubwa kimaendeleo.

Dk. Gwajima ameyasema hayo leo Desemba 8, jijini Dodoma, muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuteuliwa na Rais kuwa mbunge na kisha Waziri mteule wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Naamini wananchi wapo na sisi, nipo, nimekuja nasubiri kutumwa kazi, tujenge nchi yetu pamoja na wazalendo wote wapenda mabadiliko wanaopenda kuiona Tanzania inakwenda kwenye ngazi nyingine kwa kadri ya maono ya Rais wetu, naomba ushirikiano wenu, ushirikiano wangu mmepata,” amesema Dk. Gwajima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles