24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Tulia: Ushirikiano wa bunge na serikali siyo udhaifu

Na Faraja Masinde

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson amesema ushirikiano kati ya bunge na serikali ni wa muhimu na siyo udhaifu kama inavyofikiriwa na baadhi ya watu.

Dk. Tulia ameyasema hayo leo, Desemba 8, kwenye hafla ya uapishwaji wa wabunge Dk. Dorothy Gwajima na Mhandisi Leonard Chamlilo.

“Kwa mkutadha huo, tunamshukuru Rais Dk. John Magufuli kwamba Serikali iko tayari kusikiliza yale ambayo bunge inalishauri, singekuwa hivyo hata haya tunayoyazungumza ingekuwa ngumu, sharia bunge ingeweza kutunga lakini serikali isichukue hatua yoyote.

“Lakini kutokana na kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali na njema ndiyo maana wabunge sasa wako karibu zaidi na mawaziri n ahata hawa wanoenda kuapa kesho ni wazi kuwa ni mchango wako.

“Mfano hawa wabunge wasingeweza kupata fursa ya kuapishwa kesho kuwa mawaziri napengine isingetokea hiyo fursa labda mpaka bunge lijalo, lakini ni wewe uliyeleta hiyo hoja kwamba kuna wakati tunaichelewesha serikali sababu ya kanuni zetu.

“Lakini wewe uliliona hilo na ukafanya mabadiliko hivyo ni wazi kuwa hili ni moja ya mambo ambayo umefanya mabadiliko makubwa na chanya ambayo yataingia kwenye historia ya nchi hii, hata kama yatakuwepo maeneo ya hapa na pale lakini kazi unayoifanya Spika ni nzuri na kubwa,” amesema Dk. Tulia

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles