29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kusoma kwa njia ya mtandao kunavyopunguza gharama

Writing down some blog ideas

Na FARAJA MASINDE,

KUPANUKA kwa utandawazi kumefanya mambo mengi yafanyike kisasa zaidi, ambapo kazi mbalimbali leo hii zinaweza kufanyika kwa njia ya mtandao tu.

Kila mtu huwa ana kiu ya kusoma nje ya nchi hasa kwenye vyuo vilivyopiga hatua za kimaendeleo, nia ikiwa ni kutanua wigo wa elimu kulingana na taaluma yake.

Hata hivyo, kutokana na changamoto za kuyumba kwa uchumi, wengi hujikuta ndoto zao zikishindwa kutimia kutokana tu na kushindwa kumudu gharama za masomo husika, pia kukosa fedha za usafiri na maradhi.

Kwa sababu kama hizo, watu wengi hubaki hapa nyumbani na kuchukua taaluma zao kwenye vyuo vya nyumbani licha ya kwamba vinatajwa kuwa nyuma kitaaluma.

Changamoto inayowapata wanafunzi na kujikuta wakishindwa kutimiza ndoto zao za kusoma kwenye vyuo vya kimataifa, kwa sasa huenda ikawa imepata ufumbuzi kutokana na kukua kwa utandawazi… sasa hivi mwanafunzi anao uwezo wa kusoma kwenye vyuo vya nje ya nchi kwa njia ya mtandao.

Kwa kutumia utandawazi unaweza kusoma moja kwa moja kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya majuu, mfumo ambao unafaida lukuki.

Kwa mataifa yaliyoendelea, hii imekuwa ni njia mojawapo inayotumika zaidi kwa wanafunzi, ambapo husoma huku wakiendelea kuendesha maisha yao.

Mfumo huu unampa mwanafunzi uhuru wa kuchagua asome wapi na kwa njia rahisi ikilinganishwa na kuwa chuo moja kwa moja.

Kwani hapa hautaingia darasani, hivyo unapata muda wa kupanga kuwa usome wakati  gani na muda gani ufanye mambo yako.

Hii husaidia hata kama unafamilia, inakuwa ni rahisi kutimiza majukumu yako ya kila siku kwani unakuwa na uhuru wa kuchagua.

Kupia mtandaoni, unakuwa na uhakika wa kupata matirio, mambo ya msingi unayotakiwa kuwa nayo ni kompyuta/laptop iliyounganishwa na mtandao wa inteneti, tabiti na vifaa vingine kwa lengo moja tu la kukurahisishia kujisomea.

Kuna tofauti kubwa unapoingia darasani na unaposoma kupitia mtandaoni. Darasani usipozingatia kuandika au kumsikiliza mwalimu basi huenda ukashindwa kukumbuka au hata kupata notisi.

Pia unapata fursa ya kumfikia mwalimu kirahisi, huu ni utaratibu uliozoleka kutumiwa na walimu wengi wa vyuo hasa vile vilivyopiga hatua kubwa – wanaotumia mawasiliano ya barua pepe kama njia ya mawasiliano.

Hivyo, hapa itakuwa rahisi kwako wewe mwanafunzi kuweza kumfikia mwalimu wako moja kwa moja ikilinganishwa na kuwa shuleni ambapo unaweza usimkute ofisini hivyo ikawa ni changamoto.

Pia njia hiyo inaweza kukupa wepesi zaidi wa kupata taarifa mbalimbali ikiwamo matokeo yako na mengine kwani muda mwingi kila kitu kinakuwa kikifanyika kwenye mtandao na hivyo unakuwa wa kwanza kupata taarifa.

Faida nyingine ni kwamba hakuna gharama kubwa za masomo, ni kugharimia ada pekee tofauti na aliyeko chuoni ambaye hulazimika kulipa gharama za ziada.

Hapa unaepuka vitu kama gharama za hosteli, vitabu, usajili na mambo mengine.

Lakini pia inakuweka kwenye mazingira ambayo ni rafiki na mwalimu wako kwani hata kama ni mkali kamwe hamuwezi kukwaruzana.

Na hivyo mnajikuta mkiwa na maelewano mazuri zaidi kiasi kwamba hata pale unapoteleza inakuwa ni rahisi kukueleza kwa njia ambayo ni rafiki kuliko ukiwa darasani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles