Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Mkoa wa Kusini Unguja, umeendeleza ubabe katika mashindano ya riadha ya wanawake ‘Ikangaa Ladies First’ baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mara ya tano mfululizo.
Mshindano hayo yanayodhaminiwa ya Shirika la Maendeleo la Japani(JICA) na kuratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa(BMT), yamemalizika Novemba 26, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Katika michuano hiyo, Kusini Unguja imeubuka kinara kwa kujikusanyia medali tano ambapo nne za dhaimeongoza kwa medali nne za dhahabu na moja ya fedha.
Nafasi ya pili imekwenda kwa Kilimanjaro iliyopata medali za dhahabu tatu, fedha mbili na shaba tano, wakati Pwani imemaliza ya tatu.
akimalizia nafasi ya tatu.
Akizungumzia ubingwa huo, kocha wa timu ya Kusini Unguja, Makame Hassan Juma, amesema siri mafanikio yao ni kufanya mazoezi kwa bidii kuhakikisha wanatunza vipaji wanavyoibua.
“Miaka yote tangu mashindano haya yameanzishwa Kusuni Unguja ndiyo mabingwa. Naishauri mikoa mingine ijitume ili kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali,” amesema Juma.