28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Kusini Unguja  haikamatiki Ikangaa Ladies First

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania  Digital


Mkoa wa Kusini Unguja, umeendeleza ubabe katika mashindano ya riadha ya wanawake ‘Ikangaa Ladies First’ baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mara ya tano mfululizo.

Mshindano hayo yanayodhaminiwa ya Shirika la Maendeleo la Japani(JICA) na kuratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa(BMT), yamemalizika Novemba 26, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Katika michuano hiyo, Kusini Unguja  imeubuka kinara kwa kujikusanyia medali  tano ambapo nne za dhaimeongoza kwa medali nne za dhahabu na moja ya fedha.

Nafasi ya pili imekwenda kwa Kilimanjaro iliyopata medali za dhahabu tatu, fedha mbili na shaba tano, wakati  Pwani imemaliza ya  tatu.

 akimalizia nafasi ya tatu.

Akizungumzia  ubingwa huo, kocha wa timu ya Kusini Unguja, Makame Hassan Juma,  amesema siri  mafanikio yao ni kufanya  mazoezi kwa bidii  kuhakikisha  wanatunza vipaji wanavyoibua.

“Miaka yote tangu mashindano haya yameanzishwa Kusuni Unguja ndiyo mabingwa. Naishauri mikoa mingine ijitume ili kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali,” amesema Juma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles