30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

KUNDI LA IS LAKIRI KUSHAMBULIA BARCELONA

BARCELONA, HISPANIA

KUNDI la Islamic State (IS), limekiri kuhusika na mashambulizi mjini Barcelona nchini Hispania. Serikali ya Catalonia imesema watu 13 wamekufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya gari la mizigo kugonga watu katika eneo la watalii la Las Ramblas mjini humo.

Wakati huo huo polisi imesema imewakamata watu wawili pamoja na kuzuia shambulio la pili katika mji wa Cambril Kusini Magharibi mwa Barcelona. Hata hivyo, washambuliaji watano waliuawa kwa mujibu wa polisi ya Catalonia.

Kundi la IS kupitia shirika lake la propaganda la Amaq, limetangaza kwamba ndio wamehusika na shambulizi hilo. Taarifa hii imethibitishwa na shirika la Marekani linalokagua tovuti za makundi ya kijihadi, SITE.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa dereva wa gari aliliendesha na kutoroka kwa miguu baada ya kuwagonga watu kadhaa.

Maofisa usalama nchini Hispania wanasema watu kadhaa wamejeruhiwa kutoa huduma za dharura wakiwashauri watu kukaa mbali na eneo hilo.

Ripoti kutoka eneo hilo zinasema kuwa watu walijificha ndani ya maduka yaliyo karibu, baada ya shambulio hilo. Vikosi vya usalama na ulinzi vinaendelea kuwasaka wahusika wa shambulio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles