29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

BUNGE LAMKATALIA RAIS MUSEVENI

KAMPALA, UGANDA

HATUA ya Serikali ya Uganda kutaka kubadilisha Ibara ya 26 ya Katiba ili iwe na nguvu za kumiliki ardhi mahali popote wakati wowote, imepata pigo baada ya wabunge wa chama tawala kukataa kumuunga mkono Rais Yoweri Museveni.

Wabunge 278 kutoka chama tawala cha National Resistance Movement (NRM), wamemweleza Museveni kwamba hatua yake ya kutaka kubadilisha katiba ni sumu kwa taifa.

Rais Museveni ameambiwa kwamba hakuna namna, angeweza kuwashawishi raia kukubali kuifanyia marekebisho hayo ili kuiruhusu Serikali kumiliki ardhi kimabavu, wakati wowote, pahali popote, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Serikali.

Badala yake wabunge hao wamekubaliana kuunda kamati maalumu itakayokuwa ikishughulikia masuala ya ardhi kote nchini endapo Serikali inataka kutekeleza miradi ya maendeleo mahali popote pale.

Kamati hiyo itakuwa na muda wa siku 90 kukamilisha vikao vyake na iwapo mwenye ardhi hajaridhika, atalazimika kwenda mahakama kuu itakayosikiliza kesi kwa muda usiozidi siku 3, huku baadhi ya wabunge wakiunga mkono vitendo vya kuchoma greda zinazotumika katika uvamizi wa ardhi.

Suala kuu ni kuhakikisha kwamba miradi ya Serikali inatekelezwa kwa muda ili kuhakikisha Waganda hawapati hasara. Wabunge wote waliohudhuria kikao wamekubaliana kwamba ni lazima miradi ya Serikali itekelezwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles