27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kunani Mzee Yusuph na Khadija Kopa?

Mzee Yusuf new.jpg 2khadija kopaNA THERESIA GASPER

MANENO ya kujitamba aliyokuwa akiyatoa mwimbaji wa taarabu, Mzee Yusuph kila mara alipokwenda kupokea tuzo usiku wa juzi, yamewapa wasiwasi wadau wa muziki huo wakihoji kwanini ameonyesha kuwadharau baadhi ya waimbaji wenzake wa muziki huo.

Mwimbaji anayedaiwa kuelekezewa maneno hayo ni mkongwe wa siku nyingi, Khadija Kopa ambaye alishadai kwamba aliwahi kuonyesha njia ya kutaka kushirikiana na mwenzake huyo lakini ameonekana kumkwepa bila sababu za msingi.

Wakati Mzee Yusuph akijitapa jukwaani, Khadija Kopa alidai alimtafuta mara kadhaa ili waimbe wimbo wa kushirikiana kama mfalme na Malkia lakini mwenzake huyo amekuwa akimkwepa ishara inayoonyesha kwamba hataki kushirikiana naye ingawa hajui sababu za hilo.

“Mimi nilishamfuata Mzee Yusuph nikitaka tushirikiane tutoe wimbo kama yeye Mfalme nami Malkia, lakini mwenzangu naona kama hapendi maana amekuwa akinikwepa na wimbo tulioshirikiana ni kwa sababu ya shirika moja wapo lilitukutanisha kila mtu kwa wakati wake tukafanya kazi kwa kuwa ni ya shirika na ilikuwa inalipa, lakini kwa wimbo wetu amekuwa akinikwepa na sijui sababu zake,” alieleza Khadija Kopa.

Baadhi ya maneno aliyojinadi nayo Mzee Yusuph usiku wa juzi katika ukumbi wa Mlimani City, ni pamoja na kutaja baadhi ya majina ya wasanii walipo katika muziki huo na kutomtaja Malkia wa muziki huo, Khadija Kopa, huku akidai hawajui wasanii wengine jambo lililozua minong’ono kwa wahudhuriaji wa tuzo hizo. Katika tuzo hizo, Mzee Yusuph alinyakua tuzo tatu ikiwemo msanii bora wa kiume wa taarabu, mtunzi bora wa mwaka wa taarabu pamoja na kikundi bora cha taarabu cha Jahazi Modern Taarabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles