28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate kutoa somo kwa wasanii leo

JokateNA THERESIA GASPER

MREMBO na mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo, leo atatoa somo kwa wasanii na wadau wa sanaa katika kongamano la Jukwaa la Sanaa litakalofanyika kwenye ukumbi wa Basata jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Basata, Aristides Kwizela, alisema Jokate pamoja na mbunifu mashuhuri wa mitindo ya mavazi nchini, Asia Idarous, watatoa mada katika jukwaa hilo na watazungumzia namna ya kutumia umaarufu na vipaji vyao kukuza kipato.

“Jukwaa hili litawataka wasanii na wadu wa sanaa wachakarike, wapate mwanga na namna ya kutumia umaarufu na vipaji walivyonavyo katika kuibua miradi ya ujasiriamali na kujiongezea kipato,” alisema Kwizela.

Alisema wameamua kuweka mada hiyo lengo ni wadau wa sanaa wajifunze kutoka kwa wanamitindo hao wawili ambao wamekuwa na mafanikio makubwa katika kazi zao zinazoendana na umaarufu wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles