26.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kuiona Taifa Stars, Msumbiji Sh 7,000

Bonifance Wambura
Ofisa habari wa TFF, Bonifance Wambura

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limetangaza kiingilio cha chini kati ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Msumbiji ‘Mambas’ kuwa ni Sh 7,000 mchezo utakaochezwa Julai 20, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo tiketi zitakuwa zikitolewa kwa mfumo wa elektroniki,  kupitia M-PESA ikiwa ni mara ya kwanza mfumo huo kutumika katika mechi kubwa kama hiyo tangu mfumo huo utangazwe kuanza kutumika.

Kiingilio hicho cha Sh 7000 ni kwa ajili ya viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ambapo viingilio katika maeneo mengine vitatangazwa baadaye.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa TFF, Bonifance Wambura alisema mashabiki ili wapate tiketi wanatakiwa kutumia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha wanabonyeza 4, unaingiza namba ya kampuni 173399  kisha unaweka kiasi  7,000 kwenye namba ya kumbukumbu ya malipo na unaweka 7,000 kama kiasi cha bei ya tiketi na mwisho unaweka namba ya siri.

“Baada ya hapo utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo kwa ajili ya kuchukulia tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako,” alisema.

Vituo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre), Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho, Sheer Illutions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).

Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na ofisi za TFF (PPF Tower).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles