27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Magufuli: Mkono, Kangi ni majembe CCM

Waziri John Magufuli
Waziri John Magufuli

Benjamin Masese na Shomari Binda

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amewasifia wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba ni miongoni mwa  majembe makubwa ndani ya chama   wanaotekeleza ahadi zao katika majimbo yao.

Wabunge aliowapongeza ni Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Kangi Lugola wa jimbo la Mwibara.

Dk. Magufuli alitoa pongezi hizo alipozindua kivuko cha MV Mara ambacho kitatumiwa na wakazi wa vijiji vya Iramba na Majita huku akiwataka kukitunza   kiweze kuwasaidia katika kuinua uchumi wa maeneo yao.

Kivuko hicho kimegharimu zaidi ya Sh milioni 545  na kitakuwa kikitoa huduma  kutoka wilayani  Bunda  hadi   Busekera katika Wilaya ya Musoma Vijijini.

Alisema kivuko hicho kimepelekwa katika eneo hilo kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete pamoja na  jitihada kubwa za wabunge hao waliowasilisha hoja ya kuwapo na kivuko katika eneo hilo ili  kuondoa adha ya usafiri iliyokuwa ikiwakabili wananchi hao.

“Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea  maendeleo  yenu  na maeneo ya jirani lakini nawaonya wavuvi kutotega nyavu zao kwenye njia za kivuko.

“Nyavu hizo zikiwekwa kwenye njia ya kivuko zitasababisha kivuko kuharibika, hivyo ni jukumu la wote kuhakikisha tunakilinda  kiweze kudumu.

Dk. Magufuli alisema   kivuko hicho kina uwezo wa kubeba tani 25 ambazo ni magari manne   na abiria 50.

“Nimeambiwa nauli ilikuwa Sh 2,000 kuvuka upande wa pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki kipya ni Sh 500, wanafunzi waliovaa sare watapanda bure, watoto Sh 100,” alisema.

Hata hivyo, alisema nauli za magari na mizigo zitapangwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndiyo wasimamizi wa kivuko hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles