22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

KUBORESHA UTAWALA BORA HULETA TIJA

Na MWANDISHI WETU

BAADHI ya michango ya hoja zinazotolewa kwa kuegemea sababu za kiutamaduni na kihistoria katika kuelezea utawala bora, inafanya iwe rahisi kuangukia katika kambi ya wanaoona mabaya jambo ambalo ni kosa.

Utawala bora ni pamoja na kuwa na mikakati inayoelekea katika mageuzi yenye tija kwa jamii  kwa kuwa na uwazi unaosaidia kuuboresha na kupunguza rushwa ambavyo ni vitu muhimu  kwa maendeleo bora na uchumi kukua kwa haraka.

Kama ni suala la mageuzi yenye tija, yapo baadhi ya mambo ya msingi ambayo nchi inatakiwa kutumia kujitathmini na miongoni mwake ni kuweka wazi amana na mapato ya watu wanaogombea au walio na dhamana katika ofisi za umma.

Jingine ni kuweka wazi kura zote kwa ajili ya Bunge, kuandaa miswada na mijadala ndani ya Bunge na utekelezaji kwa makini wa sheria zilizo na masilahi, kutenganisha biashara, siasa, Bunge na huduma za umma.

Kuweka wazi mbele ya umma orodha ya mashirika ambayo yamekuwa yanaonesha  kuhonga kwenye manunuzi ya umma (kama ambavyo imeshafanywa na Benki ya Dunia) na ‘kuchapisha kile ambacho umelipa’ kwa mashirika ya kimataifa katika manunuzi.

Kutekeleza kwa ufanisi sheria za uhuru wa habari kwa kuwezesha kwa urahisi kufikiwa kwa taarifa za Serikali na hata uhuru wa habari ikiwemo intaneti na mitandao ya jamii.

Uwazi kwenye fedha za umma za  bajeti kuu na bajeti za serikali za mitaa. Aidha, Serikali  inatakiwa kutoa taarifa ya malipo kwa  mashirika ya kimataifa katika sekta ya uzalishaji viwandani na kuwa na mikutano ya wazi inayojumuisha wananchi.

Kubainisha kwa uwazi mikakati ya utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa na kuweka programu za wazi ndani ya miji na ngazi za mikoa, ikiwa ni pamoja na kuweka bajeti wazi katika mikutano ya wananchi.

Ukweli ni kwamba yapo maeneo ambayo yanaangukia nje ya mamlaka za taasisi hizo, kama vile kuboreshwa kwa chaguzi  huru na za  haki za vyama vingi.

Nchi tajiri ni wapiga debe wazuri wa suala la utawala bora lakini hazioneshi utekelezaji sahihi katika kutoa misaada yake na hata kutekeleza ahadi za biashara huria.

Kama nchi tajiri zikiboresha uwazi hasa inapotokea nchi maskini kuibiwa, basi upigaji debe wao utakuwa na tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles