24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

DIWANI CCM KIKAANGONI KWA KUIPIGIA KURA CHADEMA

Na SHOMARI BINDA

DIWANI wa Kata ya Suguti, Denis Ekwabi (CCM), ameingia matatani baada ya kutuhumiwa kumpigia kura mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.

Ekwabi pia aliwa kushika nafasi ya makamau mwenyekiti katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma,

Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma, Benard Ghati, alisema diwani huyo amefanya kitendo ambacho hakikubaliki ndani ya chama kwa kuwa huo ni usaliti.

Alisema yeye kama katibu wa chama aliyekuwapo kwenye uchaguzi huo anakilani kitendo hicho.

Alisema    tayari limelifikisha jambo hilo katika vikao ambavyo vitatoa uamuzi juu ya kitendo kilichofanywa na diwani huyo.

Katibu huyo alisema katika uchaguzi huo ambao uliwajumuisha madiwani wa CCM na Chadema walikuwa  26, CCM walikuwa 22 na Chadema wane.

Alisema baada ya kura kupigwa mgombea wao alipata kura 21 na mgombeawa Chadema alipata kura tano hatua ambayo iliwafanya kuhoji diwani gani aliyempigia kura mpinzani.

“Baada ya kuhojiana mwanzoni diwani huyu alikana kupiga kura upinzani lakini baadaye yeye mwenyewe alikiri kufanya hivyo.

“Sasa kwa kuwa zipo taratibu ndani ya chama jambo hili tutalipeleka kwenye vikao husika   viweze kutoa uamuzi,”alisema Ghati.

Katika uchaguzi huo   Diwani wa CCM, Ibrahim Malima (CCM), alishinda kwa kupata kura 21 na mgombea wa Chadema, Benjamini Peter, alipata kura tano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles