25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

KUBENEA ASHIKILIWA NA POLISI, KUSAFIRISHWA DODOMA LEO

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), anashikiliwa na polisi Kituo cha Oysterbay akisubiri taratibu za kusafirishwa kuelekea Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Kubenea anatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo kesho, mjini Dodoma kwa agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyezitaka kamati hiyo na ile ya Ulinzi na Usalama kumhoji mbunge huyo kwa kile alichokisema kuwa Spika ni mwongo kwani ametaja idadi chache ya risasi alizoshambuliwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wiki iliyopita.

Kubenea alifika hospitalini hapo leo asubuhi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wakimsubiri amalize matibabu.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Kubenea amethibitisha kukamatwa na polisi saa nne asubuhi leo, akiwa nyumbani kwake lakini aliwaambia anaelekea hospitali kupima kipimo cha MRI ambapo alifanya huku polisi wakiwa wanamsubiri na baada ya kumaliza kufanyiwa uchunguzi waliondoka naye na kumpeleka moja kwa moja kituo cha  Polisi Oysterbay, Mkoa wa Kinondoni.

“Nipo kituoni nasubiri kuandaliwa taratibu za safari kwenda Dodoma lakini hali yangu kiafya bado si nzuri, nimewaambia ninaumwa wamesema wao wamepewa taarifa kuwa wanikamate hawana mamlaka mengine hivyo wanachokifanya ni kunipeleka Dodoma kama walivyoagizwa,”amesema Kubenea.

Hata hivyo, mmoja wa wanasheria wa Chadema, amesema daktari ameshauri asisafiri kwa kutumia barabara kutokana na afya yake lakini usafiri uliopo ni magari pekee.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Mulilo amekataa kuzungumzia suala hilo lwa madai kuwa si msemaji.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Ni Watanzania hawa, Ni viongozi wetu hawa, Ni ndugu zetu hawa, Ni baba zetu hawa, ni waume zetu hawa, Wajomba zetu, jirani zetu, Watani zetu, Tunaanza kuitambua nguvu , ushujaa wa wapinzani. Tishio kwa serikali. Mbona hatuwanyanyasi Wachina, Wazungu, Wahindi, na wengineo. Tutaheshimika vipi nyumbani kwetu kama Watanzania kwa Watanzania hatujaliani, tunavisasi,tunanyanyasana, hatuthaminiani,hatupendani,tunauana,ni sisi kwa sisi. Nyumbani kwetu. Wapi tena tutaheshimika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles