23 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

MOURINHO AANZA KUMCHOKOZA GUARDIOLA

MANCHESTER, England

NI kama kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, ameanza kulewa kwa matokeo mazuri ya kikosi chake msimu huu baada ya kumtupia dongo hasimu wake wa siku nyingi, Pep Guardiola.

Makocha hao wamekuwa wapinzani wakubwa kwenye ulimwengu wa soka na uhasama wao huo ulianza miaka kadhaa iliyopita walipokuwa La Liga wakizinoa Real Madrid na Barcelona.

Hata hivyo, kauli ya Man United baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Everton juzi, inaonekana kuuamsha upinzani wao huo ambao ulionekana kupungua tangu walipotimka Hispania, Mourinho akarejea Chelsea na Guardiola akachukuliwa na Bayern Munich.

Mourinho amesema juzi hakupoteza hata sekunde moja kuifikiria timu hiyo ambayo ilicheza Jumamosi na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Watford.

Mourinho alidai kuwa wakati wa mchezo wake dhidi ya Everton, hakuwa amepoteza hata sekunde moja kuufikiria ushindi wa Guardiola dhidi ya Watford.

Dhidi ya Everton, Man United walipata ushindi kupitia mabao ya Antonio Valencia, Henrikh Mkhitaryan, Romelu Lukaku na Anthony Martial, huku matatu yakifungwa katika dakika saba za mwisho wa mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.

“Sikutumia hata sekunde moja kuifikiria Manchester City,” alisema Mourinho kuwaambia waandishi wa habari. Nilikuwa nazifikiria Tottenham, Arsenal, Chelsea na Liverpool,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles