26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Korosho kaa la moto, Serikali yatoa siku Nne kwa wanunuzi 

                                    Bethsheba Wambura



Wanunuzi 35 walijoandikisha kununua korosho wamepewa siku Nne na Serikali wawe wamepeleka barua katika Ofisi ya Waziri Mkuu wakionesha  kiasi cha tani wanazohitaji na lini watazichukua .

Tamko hilo la Serikali limetolewa  leo Ijumaa, Novemba 9, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa uamuzi wa  Serikali kuhusu ununuzi wa zao la korosho ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Amesema baada ya kupita siku hizo Serikali italazimika kufuta usajili kwa wote waliojisajili kununua zao hilo kwa sababu walikubaliana kwenda kununua inayvoonekana sasa ni kumkomoa mkulima kitu ambacho imesema haitakubaliana nacho.

“Hivyo wanunuzi waliojiandikisha wakiwemo na wale ambao wamekuwa wananunua kwenye minada lakini kwa kiasi kidogo, wahakikishe ndani ya siku hizo kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu saa 10 alasiri wawe wameleta barua na ofisi yangu ipo wazi saa 24.

“Mwenye nia ahakikishe katika siku hizo nne iwe ndio mwisho wa kununua korosho na waandike barua kwani ofisi yangu ipo wazi saa 24 wana nafasi ya kuleta barua wakati wowote wakionesha nia yao na kiwango wanachokihitaji. Zaidi ya hapo Serikali haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena,” amesema, “amesema.

Waziri Mkuu amesema kwenye msimu wa ununuzi wa korosho wa mwaka huu, walishuhudia kusuasua kwa minada, ambapo Serikali ilikutana na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichoongozwa na Rais Dk John Magufuli ambapo walikubaliana kununua kwa bei inayoanzia sh 3,000 na kuendelea.

“Mjadala ulikuwa wa wazi na wafanyabiashara wenyewe walipendekeza bei ambayo ilikuwa inaanzia sh. 3,000, hata hivyo baada ya kikao hicho ununuzi katika minada umeendelea kusuasua na hata tani zilizokuwa zikinunuliwa zilikuwa kidogo sana sisi tunaiona hali hii kama mgomo baridi ambao si sawa kwani malengo yetu sisi na sekta binafsi ni kumfanya mkulima apate bei nzuri, “ amesema Majaliwa.

Hata hivyo Serikali imewataka wananchi hususani wakulima wa korosho nchini kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu wakati ikiendelea kushughulikia suala hilo.

 

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles