27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MCT, asasi za kiraia walaani kukamatwa kwa waandishi wa kigeni

                     Bethsheba Wambura, Dar es Salaam



Kitendo cha kukamatwa kwa kwa maafisa wa Kamati ya Ulinzi wa Waandishi (CPJ)  Angela Quintal (raia wa Afika Kusini) na Muthoki Mumo (raia wa Kenya) kimelaaniwa vikali na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)  na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mafisa hao walikamatwa Jumatano Novemba 7, 2018 saa Nne na Nusu usiku katika hoteli  ya Southern Sun iliyopo jijini Dar es Salaam na watu watatu ambao mmoja wao alijitambulisha kuwa ni Ofisa wa Idara ya Uhamiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba 9, Kaimu Katibu Mkuu wa MCT Pili Mtambalike amesema baada ya kukamatwa maafisa hao walipelekwa kuhojiwa na walinyang’anywa Kompyuta mpakato’Laptop’, simu na hati zao za kusafiria ‘Passport’,  baadae maafisa hao walirudishiwa simu zao.

Amesema pamoja na kurudishiwa simu zao ujumbe uliotumwa katika ukurasa wa Twitter wa Angela ulisema kuwa wameshaachiwa huru ulikuwa wa kughushi na si wa mmiliki halali akaunti hiyo na hati zao za kusafiriwa ziliendelewa kushikiiwa hadi Alhamis Novemba 8, juhudi zilifanywa na Ofisi za balozi husika na  wadau zilizopelekea maafisa hao kurudishiwa ‘Passport’ zao.

“Kutokana na hofu zao wawawakilishi wa Balozi za nchi wanazotoka maafisa hao waliwashauri waondoke na uongozi wa CPJ umethibitisha wawili hao wamaeshapndoka nchini.

“Ikumbukwe kwamba maafisa hao walikuja mchini kwa minajili ya kungalia hali ya usalama wa waandishi wa habari, hata hivyo taarifa zilizotoka kwa msemaji wa Idara ya Uhamiaji zilisema wawili hao walikiuka masharti ya viza zao ambapo walipewa za matembezi lakini wao walikuwa wanahoji waandishi wa habari, “ amesema Pili.

Kwa upande wake Mratibu Taifa wa THRDC Onesmo Olenguruwa amesema woa kama wattezi wa haki za binadamu wamesikitishwa na namna waliyowakamata maafisa hao kwani walikuja nchini kihalali na hata baada ya kuachiwa huru hakuna masharit yoyote waliyopewana kuambiwa waendelee na shughuli zao.

“Tunaviomba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama  vifanye kazi zake kwa weledi na kwa mujibu wa sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo nchi imeridhia ili kudumisha amani,tunaiomba Serikali yetu iulinde kwa nguvu zote uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine ili kuboresha taswira yetu iliyojengeka kimataifa kuwa sisi ni kisiwa cha amani, “.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles