Na KULWA MZEE – DAR ES SALAAM
BALOZI wa Korea Kusini nchini, Geum-Young Song, amesema serikali yake inakusudia kuanzisha viwanda vya kutengeneza na kuunganisha magari nchini.
Balozi Song alisema hayo jana alipokutana na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi kwa mazungumzo.
Balozi huyo alisema Korea Kusini inaomba msaada wa Mwenyekiti, Dk. Reginald Mengi katika kufanikisha ujenzi wa viwanda hivyo.
Dk. Mengi alisema walishakuwa na mpango wa kuanzisha mradi wa kiwanda hicho na Syri Lanka lakini kwa kuwa Korea wameonyesha ushirikiano watashirikiana nao kufanikisha malengo hayo.
Alisema Serikali ya Korea imeonyesha nia ya kusaidia katika sekta ya viwanda hasa kwenye uwekezaji wa kiwanda cha kuunganisha magari hayo na yeye yupo tayari kuwasaidia.
“Uchumi wa viwanda unahitaji wataalamu wengi.
Naamani kupitia ushirikiano huu tunaweza kupata na haraka iwezekanavyo ndoto ya Rais ya kufikia kwenye uchumi wa viwanda.
“Vipo vitu vingi vinaingia kutoka Korea kama televisheni, simu za mkononi na vitu vingine vya mawasiliano, tuanze hapa nyumbani kutengeneza vya kwetu,” alisema.