22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

KONGA MKURUGENZI MPYA NHIF

Na MWANDISHI WETU – Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amemteua Bernard Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema uteuzi huo ulianza tangu Agosti 9, mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Konga alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu mwaka jana iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa Emannuel Humba kustaafu.

Awali nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Michael Mhando ambaye alitumbuliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu kwa tuhuma za udanganyifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles