Na Mohammed Ulongo
Wafanyabiashara nchini wameomba punguzo la kodi la asilimia tatu katika biashara  wanazozifanya ili waweze kupata faida, wakidai kodi iliyopo inawabana kutokana na ugumu wa biashara.
Hayo yamesemwa leo na wafanyabiashara walipokutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Pombe Magufuli, katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kueleza changamoto zinazowakabili.
Walisema wingi wa kodi ndiyo chanzo kikuu cha rushwa kwani baadhi ya wafanyabiashara hubuni mbinu za kuzikwepa mamlaka husika .
Aidha, walimuomba Rais Magufuli kufuatilia watumishi wa umma kwani baadhi yao wamekuwa wakikiuka maadili ya utumishi .
 Sambamba na hilo, wafanyabiashara hao walimshahuri Rais Magufuli kuboresha Kiwanja cha Ndege kilichokopo ndani ya Mbuga ya Katavi ili kuimarisha sekta ya utalii nchini.