29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha mpya Simba huyu hapa

Untitled-2NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

ZIKIWA zimebaki siku  12 ili klabu ya soka ya Simba imtambulishe rasmi kocha mkuu wa timu hiyo, klabu hiyo  huenda ikanasa kwa mmoja  kati ya makocha watatu wa kimataifa  kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho.

Makocha hao ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Sierra Leone, Sellas Tetteh, kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Kenya, Bobby Williamson na kocha wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Frank Nuttall.

Simba  tangu Januari 12 mwaka huu inahaha kumtafuta kocha mkuu wa timu hiyo, baada ya kumfukuza kocha wake mkuu, Dylan  Kerr, ambapo baadaye timu hiyo ilipewa Jackson Mayanja kama kocha msaidizi ili kuisaidia kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

Awali klabu hiyo ilinasa  mikononi mwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zimbabwe, Kalisto Pasuwa, kabla ya mipango kuvurugika baada  ya  timu yake  kufuzu michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Gabon.

Taarifa kutoka nchini Ghana zinadai kwamba, Tetteh alitarajia kutua nchini  Juni 17 mwaka huu, kwa ajili ya mazungumzo  ya mwisho na kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.

“Tetteh anatarajia kutua Tanzania kwa ajili ya kumalizia mazungumzo na viongozi wa klabu ya Simba, ili aweze kukinoa kikosi hicho,” ilisema taarifa hiyo kutoka Ghana.

Kocha huyo ambaye mwaka 2015 Shirikisho la Soka  Afrika  (CAF) lilimtaja kama kocha bora wa mwaka, anakumbukwa zaidi wakati alipokuwa kocha wa vijana wa taifa hilo chini ya umri wa miaka 20 ambao waliibuka Mabingwa  wa Dunia mwaka 2009 nchini Misri.

Pia Tetteh, mwaka 2008 aliwahi kuwa mwangalizi wa  timu  ya taifa ya nchi hiyo ‘Black Stars’, kabla ya kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ na baadaye kuwa kocha wa muda wa timu ya Taifa ya Sierra Leone.

Hata hivyo, mkataba wa awali wa kocha huyo ulimazika Oktoba mwaka jana, baada ya timu yake kufungwa na Chad na kuondolewa katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia linalotarajiwa  kufanyika mwaka 2018 Urusi.

Hata hivyo, Shirikisho la soka la nchini humo lipo kwenye mchakato wa kumwongezea muda kocha huyo ili awe kocha wa kudumu.

Mbali ya kocha Teteh, Simba ipo kwenye mazungumzo Nuttall pamoja na Bobby  ambapo  inadaiwa wapo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo ya awali.

Simba ilimaliza nafasi ya tatu msimu uliopita ikiwa nyuma ya Azam FC iliyomaliza nafasi ya pili na wapinzani wao Yanga ambayo ilifanikiwa kuibuka na ubingwa wa ligi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles