27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Barcelona awahofia Man United

BARCELONA, HISPANIA

KOCHA wa timu ya Barcelona, Ernesto Valverde, amesema kupangiwa Manchester United katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kitu kizuri lakini anawahofia kutokana na ubora wao wa siku za hivi karibuni.

Droo ya kuelekea michezo hiyo ilipangwa tangu Ijumaa wiki iliyopita, huku Manchester United wakijikuta wakipangwa na wabaya wao wa mwaka 2009 na 2011, ambapo mara zote mbili Man United ilichezea kichapo huku Barcelona ikiwa chini ya kocha, Pep Guardiola.

Manchester United ipo katika kiwango kizuri tangu ichukuliwe na kocha, Ole Gunnar Solskjaer, kutoka kwa Jose Mourinho Desemba mwaka jana.

Timu hiyo imeweza kuwaondoa mabingwa wa soka nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain, baada ya mchezo wa kwanza Paris Saint-Germain kushinda kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Old Trafford, kabla ya United kwenda kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano huko nchini Ufaransa, ambapo walishinda kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kuingia hatua hiyo ya robo fainali kwa idadi kubwa ya mabao ya ugenini.

Michezo hiyo ya robo fainali inatarajiwa kupigwa mapema mwezi ujao, hivyo kocha huyo wa Barcelona anaamini ratiba yake itakuwa ngumu kwa kipindi hicho kutokana na michezo wanayoshiriki, ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Hispania na Copa del Rey.

“Itakuwa ngumu, tunajua kila timu ambayo imeingia katika hatua hiyo ina matumaini makubwa ya kufanya vizuri. Timu zote zinastahili kuwa hapo zilipo, Man United ina historia kubwa kwenye michuano hiyo mikubwa, naweza kusema ni timu kubwa kama sisi, hivyo ni mchezo ambao utakuwa na ushindani mkubwa na kuvutiwa, lakini utakuwa mgumu sana kutokana na ubora wa wapinzani, kikubwa ni matokeo kwa upande wowote.

“Wamefanya vizuri kwa mchezo wa ugenini dhidi ya PSG, hivyo lazima tuwe makini kwa kiasi kikubwa. Hawakati tamaa mapema hata kama wana wachezaji wengi majeruhi kama ilivyo kwa mchezo dhidi ya PSG, hivyo na sisi lazima tuwe makini na tujiandae kwa hilo,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles