24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha aahidi makubwa Iceland

Heimir Hallgrimsson
Heimir Hallgrimsson

NICE, UFARANSA

BAADA ya Iceland kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Euro 2016, kocha wa timu hiyo, Heimir Hallgrimsson, ameahidi makubwa katika hatua ijayo.

Timu hiyo imeingia hatua hiyo baada ya kuitoa England kwa mabao 2-1, hivyo kocha huyo amedai kwamba anatarajia kuwashangaza wapenzi wa soka kuanzia hatua ya robo fainali.

“Tulikuwa nyuma kwa bao 1-0, lakini tuliweza kusawazisha na kuongeza, hivyo ninaamini huo ni mwanzo mzuri wa kuonesha nini tunatarajia kukifanya katika michezo ijayo.

“Wapinzani walikuwa na uwezo mzuri na walitutisha baada ya kupata bao la mapema, lakini katika soka hakuna mtu ambaye anajua nini kinaweza kutokea ndani ya dakika 90, hivyo tunajivunia kufika hatua ya robo fainali.

“Hakuna ambaye alidhani kama tutaweza kufanya hivyo, lakini nataka kuwaeleza wadua na wapenzi wa soka kwamba Iceland inatarajia kuwashangaza katika michuano hii, kuna mambo makubwa yanakuja zaidi ya tuliyoyaonesha.

“Tunajiamini na ndio maana tupo hapa kwa sasa, ninaamini kama unataka kuwa bora unatakiwa kuwa tayari nafasi ikipatikana, hivyo wachezaji wangu wapo tayari kwa hilo,” alisema Hallgrimsson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles